Jumatatu 23 Februari 2026 - 11:40
Wapalestina 80,000 waswali Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa

Hawza/ Takribani Wapalestina 80,000, licha ya hatua za kuzuia na masharti makali ya utawala wa kinyama wa Israel kwa lengo la kupunguza upatikanaji — hasa kwa waumini kutoka Ukingo wa Magharibi — waliswali Swala ya kwanza ya Ijumaa ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Msikiti wa Al-Aqsa na viwanja vyake.

Kwa mujibu wa kitengk cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, pamoja na vitisho na licha ya kwamba makumi ya Wapalestina walizuiwa kufika Al-Quds inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni, na pia waandishi wa habari na timu za kitabibu kukumbana na vizuizi katika kituo cha ukaguzi cha Qalandia, bado Wapalestina waliswali kwa pamoja Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa.

Askari wa utawala wa Israeli pia walizuia kabla ya Swala kuingia kwa vijana wa kiume katika msikiti huo, na wakaweka ukaguzi mkali kuhusu uingizaji wa vyakula; hata hawakuruhusu familia kubeba vyakula vichache walivyokuja navyo kwa ajili ya kufuturu.

Makundi ya Kipalestina na yaliyojikita katika mji wa Jerusalem yalitoa wito wa kuongezwa kwa umoja wa wananchi na kuhimiza watu wengi zaidi kuelekea Msikiti wa Al-Aqsa katika mwezi wa Ramadhani. Pia waliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi zaidi katika eneo hili ili kukabiliana na kuongezeka kwa hatua za Israeli, ambazo zinalenga kuufanya msikiti ubaki bila waumini na kuunda pengo kati ya Msikiti wa Al-Aqsa na Waislamu wa Palestina.

Chanzo: Kituo cha Taarifa cha Palestina

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha